Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limetangaza kufuta ratiba ya mechi za nusu fainali michuano ya ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho kutokana na changamoto ya ugonjwa wa corona
Hakuna tarehe rasmi iliyotangazwa kwa ajili ya mechi hizo kupigwa
Hatua hiyo ni mwendelezo wa kusitishwa kwa shughuli za soka kutokana na janga la corona
Mwezi uliopita CAF ilifuta ratiba ya mechi za kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya AFCON 2021 pamoja na ile ya michuano ya CHAN iliyopaswa kufanyia nchini Cameroon kuanzia wiki iliyopita
Ni wazi CAF watalazimika kufanya mabadiliko mengine ya kalenda ya michuano yake ambayo imeathiriwa na corona
ADVERTISE HERE