Uongozi wa klabu ya Kagera Sugar umedai kuwa hauko tayari kumuachia mkufunzi wao Mecky Mexime akajiunge na Yanga
Hivi karibuni Mexime alifichua kuwa na mkataba wa Yanga ambao alikuwa akisubiri kuusaini pengine kujiunga na mabingwa hao wa kihistoria msimu ujao
Mabosi wa Kagera Sugar wamedai kuwa wameboresha maslahi ya nahodha huyo wa zamani timu ya Taifa hivyo wana matumaini ataendelea kubaki nao
Inafahamika uongozi wa Yanga ulikuwa mbioni kukamilisha dili la Mexime ili msimu ujao asaidiane na Mbelgiji Luc Eymael
Kuhusu nafasi ya kocha msaidizi Charles Mkwasa, atakuwa Mkurugenzi wa ufundi
ADVERTISE HERE