Kikosi cha Yanga jana jioni kimefanya mazoezi katika uwanja wa Namfua ambao utatumika kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa tisa dhidi ya Singida United baadae leo.
Ari ya wachezaji iko juu pengine kuliko hata ilivyokuwa kwenye mchezo uliopita dhidi ya watani wa jadi, Simba.
Kocha George Lwandamina amesema timu yake imefuata alama tatu mkoani Singida na sio matokeo mengine.
Shamrashamra za mashabiki hapa mjini ni kubwa, tangu saa 12 asubuhi walianza kumiminika uwanjani.
Papi Tshishimbi, Ibrahim Ajib na Obrey Chirwa ndio habari ya hapa leo.
Mashabiki hata wale wanaojinasibu kuishabikia Singida United wanahamu ya kuwashuhudia wakali hao wa kikosi cha Yanga.

ADVERTISE HERE