Molinga aipigia hesabu michuano ya kombe la FA

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Apr 2020
Molinga aipigia hesabu michuano ya kombe la FA

Mshambuliaji wa Yanga David Molinga amesema anaamini kikosi cha timu hiyo kina nafasi ya kushiriki michuano ya CAF msimu ujao hasa kupitia mashindano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)

Kimahesabu, Yanga ina nafasi finyu ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu baada ya kuzidiwa alama 20 na vinara wa ligi hiyo Simba

Molinga amesema kama wachezaji hawatakubali kumaliza msimu bila ya kuwa na kitu hivyo watapambana kwenye mechi zilizosalia huku pia wakiweka mkazo kwenye michuano ya kombe la FA

"Kwa hali ilivyo, hatuonekani kuwa na nafasi ya kutwaa ubingwa msimu huu, hatujakata tamaa kwani kwenye mpira lolote linaweza kutokea," amesema

"Lakini nafasi nzuri kwetu kupata tiketi ya kushiriki michuano ya Kimataifa ni kupitia kombe la Shirikisho. Kwani tumekuwa na mwenendo mzuri kwenye michuano hii na kila mchezaji ana kiu kuona tunafanikiwa kuwa mabingwa"

Bado anataka kubaki Yanga

Katika hatua nyingine, Molinga amesema anaamini uongozi wa Yanga utampa nafasi ya kuendelea kuwatumikia mabingwa hao wa kihistoria pale mkataba wake utakapomalizika mwezi August

Molinga amedokeza kuwa ana ofa kutoka vilabu vingine ndani ya Afrika lakini kipaumbele cha kwanza anaipa Yanga klabu anayoitumikia sasa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
2h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
11h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’