Wamepaniki? mbona shughuli ndio imeanza

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Apr 2020
Wamepaniki? mbona shughuli ndio imeanza

Baada ya GSM kurudi kwa kishindo na kutangaza hali ya hatari kuelekea msimu ujao, hofu imetanda upande wa pili huko Msimbazi ambako baadhi ya nyota wamegoma kuongeza mikataba

Zilizochini ya kapeti ni kuwa GSM imejipanga kulipa kisasi kwa kuwan'goa nyota muhimu wa timu hiyo

Inafahamika mwezi uliopita Simba ilijaribu kumnasa kiungo mshambuliaji wa Yanga Bernard Morrison kabla ya GSM kushitukia mchezo na kumpa mkataba mpya wa miaka miwili

Jana GSM wamefanikiwa kumuongeza mkataba nahodha wa timu hiyo Papy Tshishimbi ambaye pia kulikuwa na tetesi kuwa Simba walikuwa wanamtaka

Baada ya kufanikiwa kuwapa mikataba wachezaji hao, mabosi wa GSM wamesema sasa ni zamu yao kupata maumivu

Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amedokeza kuwa GSM wako tayari kumnunua mchezaji yeyote ndani ya nchi ambaye amependekezwa na kocha Luc Eymael na mshahara wake ni chini ya Tsh Milioni 40! hapa tatizo ndipo linapoanzia

Inaelezwa mpaka sasa viongozi wa Simba wanahaha kumpata kiungo wao Clatous Chama ambaye amejichimbia kwao Zambia na mkataba wake unaisha mwezi Juni

Lakini zipo taarifa za chinichini kuwa tayari GSM wameshamaliza kazi kwa Mzambia huyo!

Miongoni mwa nafasi ambazo Yanga imejipanga kusajili ni winga wa kulia

Pamoja na kumuwania Tusila Kisindo wa AS Vita, Yanga wamemuweka kwenye tajeti Deo Kanda anayecheza kwa mkopo Simba akitokea klabu ya TP Mazembe

Mkataba wa Kanda na TP Mazembe unamalizika mwishoni mwa msimu, hivyo Yanga ina nafasi ya kumnasa nyota huyo kama itatoa dau nono

GSM wametenga zaidi ya Bilioni 1.5 kwa ajili ya usajili, hivyo suala la fedha sio tatizo tena

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
21m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’