Afisa Mhamasishaji wa klabu ya Yanga Antonio Nugaz amesema ni wakati wa wapenzi, wanachama na mashabiki wa klabu ya Yanga kushikana kuelekea mabadiliko
Nugaz amesema jambo hilo jema linapaswa kuwaweka pamoja Wanayanga kwa maslahi mapana ya klabu yao
"Ni wakati wetu sasa wanachama,wapenzi na mashabiki wa Young Africans Sc kuwa pamoja na lengo letu liwe moja"
"Tushikamane kisawasawa kwa sababu hivi karibuni tunakwenda kwenye mabadiliko ya kweli na yenye tija kwa maslahi mapana ya Timu ya Wananchi."
"Insha Allah Nina imani kubwa sana ndani ya Miaka 5 ijayo YANGA itakuwa miongoni mwa timu tano zenye uwezo (Kifedha,kisoka,kimfumo) na nguvu barani Afrika na za mfano wa KUIGWA kuliko timu yeyote Afrika Mashariki na Kati na kuanzisha “Mwananchi Foundation” yenye uhalisia na mantiki halisi ya Timu ya Wananchi ili kurudisha kwa jamii kile kidogo kinachopatikana"
"Kikubwa ni Subra na imani na Uongozi chini Mwenyekiti Dkt Mshindo Msolla na Katibu Mkuu wetu Dkt David Ruhago na uwepo wa Brand Chapa Gsm kwenye kuchagiza mabadiliko ambao wao Gsm ndio wanayafadhili na ndio chachu ya kile tunachokilenga Yanga Sc"
"Shukran sana Sportpesa Mdhamini wetu mkuu , Ahsante sana Taifa Gas, Azam tv,Afya Drinking na Kongole Chapa Gsm Mdhamini,mhisani,Mfadhili"