Yanga na GSM wayamaliza

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Apr 2020
Yanga na GSM wayamaliza

Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amesema uongozi wa timu hiyo umemaliza tofauti iliyojitokeza na wadhamini wao kampuni ya GSM

Akizungumza mapema leo katika Mkutano wa pamoja na GSM, Dk Msolla amesema GSM wataendelea na majukumu yao kama ilivyokuwa mwanzo

"Tunatambua na kuthamini mchango ambao wenzetu GSM wamekuwa wakitoa kwa klabu yetu. Baada ya changamoto iliyojitokeza siku chache zilizopita, sisi kama uongozi wa Yanga tulichukua hatua kwa mujibu wa taratibu zetu na baadae tuliomba kukutana na wenzetu GSM"

"Nashukuru kikao chetu killikwenda vizuri na leo tunatangaza rasmi kuwa GSM wataendelea na majukumu yao. Wataendelea kutimiza wajibu wao kulingana na mkataba tulioingia nao. Lakini pia wataendelea kufanya yale waliyokuwa wakiyafanya ambayo sio sehemu ya mkataba," alisema Dk Msolla

Naye Mkurugenzi wa uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said amesema wao ni wanafamilia wa Yanga hivyo wataendelea na yale yote waliyokuwa wakiyafanya lengo likiwa kuhakikisha wanaitoa Yanga hapa ilipo

Mhandisi Hersi amesema wataendelea kushirikiana na uongozi wa Yanga pamoja na Mwanayanga yeyote mwenye mapenzi mema na klabu hiyo

Amesema sehemu kubwa ya kazi wanayoifanya kwa Yanga wanajitolea kwa sababu wanaipenda Yanga

Amewakaribisha wadau wengine wote ambao wangependa kuiona Yanga inasonga mbele waungane nao

Hersi amesema baada ya kukosa ubingwa kwa misimu mitatu, amewataka wanayanga kuweka malengo ya kutwaa ubingwa msimu ujao

Amesema Yanga inatarajiwa kuwa na mabadiliko makubwa ikiwemo kusajili wachezaji wapya ambao wataweza kutimiza azma hiyo ya kushinda ubingwa msimu ujao

"Hili nataka niliingie vichwani mwa Wanayanga wote. Baada ya kukosa ubingwa kwa misimu mitatu, msimu ujao ni zamu yetu kutwaa ubingwa. Tunaanza mikakati mapema kwa kuboresha timu yetu ikiwemo kusajili wachezaji wenye uwezo na kuwatengenezea mazingira mazuri wachezaji ambao tutaendelea kubaki nao"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’