Nyoni, Mzamiru waondolewa kikosi cha Stars

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
4 Nov 2017
Nyoni, Mzamiru waondolewa kikosi cha Stars
Kocha wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Salum Mayanga amewaengua kwenye kikosi chake wachezaji wawili wa Simba, beki Etasto Nyoni na kiungo Muzamil Yassin kuelekea mchezo wa kirafiki dhidi ya Benin wiki ijayo.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas amesema wachezaji hao wameenguliwa kutokana na kutolewa kwa kadi nyekundu katika mchezo uliopita dhidi ya Malawi Oktoba 7, mwaka huu Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Lucas amesema katika utaratibu wake mpya, Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) linaagiza mchezaji anayeonyeshea kadi nyekundu hata katika mchezo usio wa mashindano, asitumike katika mchezo unaofuata.

“Sasa baada ya kupokea barua ya FIFA ikituzuia kuwatumia wachezaji hao katika mchezo ujao dhidi ya Benin, kocha amefanya mabadiliko hayo madogo,”amesema Lucas.

Lucas amesema kwamba baada ya kuenguliwa kwa Nyoni na Yassin, Mayanga amewaita viungo Mudathir Yahya kutoka Singida United na Jonas Mkude kutoka Simba SC.

Baada ya kucheza nyumbani mfululizo mechi za kirafiki za kimataifa, Taifa Stars sasa itatoka mwezi ujao kwenda Benin kucheza na wenyeji Novemba 11, mwaka huu na kikosi cha wachezaji 24 kitaingia kambini Novemba 5 mjini Dar es Salaam kabla ya kusafiri Novemba 9 kwenda Benin tayari kwa mchezo huo.

Kikosi kamili cha Taifa Stars sasa ni makipa; Aishi Manula (Simba SC), Peter Manyika (Singida United) na Ramadhani Kabwili, mabeki Boniphace Maganga (Mbao FC), Abdi Banda (Baroka FC/Afruka Kusini), Gardiel Michael (Yanga), Kevin Yondan (Yanga), Nurdin Chona (Prisons) na Dickson Job (Mtibwa Sugar).

Viungo ni Himid Mao (Azam FC), Mudathir Yahya (Singida United), Hamisi Abdallah (Sony Sugar/Kenya), Jonas Mkude (Simba), Raphael Daudi (Yanga), Simon Msuva (Difaa), Shiza Kichuya (Simba), Ibrahim Hajib (Yanga), Mohammed Issa (Mtibwa), Farid Mussa (Tenerife/Hispania) na Abdul Mohammed (Tusker/Kenya) na Abdul Mohammed (Tusker/Kenya)

Washambuliaji ni Mbwana Samatta (KRC Genk/Ubelgiji), Mbaraka Yussuf (Azam FC), Elias Maguri (Huru) na Yohanna Nkomola (Huru).
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
8h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
16h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
19h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
20h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
22h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →