Jinsi Kisinda alivyopata ulaji Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Apr 2020
Jinsi Kisinda alivyopata ulaji Yanga

Dakika 847 za michezo ya kimataifa alizocheza winga Mkongo wa AS Vita, Tuisila Kisinda, zimeonekana kuwashawishi vilivyo Yanga ambayo imeonyesha nia ya kumsajili msimu ujao.

Yanga kwa sasa inataka kuhakikisha inafanya usajili wa wachezaji wazuri wa kimataifa kwa ajili ya kukiboresha kikosi chao haswa katika eneo la ushambuliaji ambapo kumekuwa na idadi ndogo ya mabao msimu huu.

Kisinda akiwa na AS Vita katika michezo ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu, amefanikiwa kucheza michezo 13, huku akifunga bao moja na kutoa pasi tatu za mabao.

Winga huyo katika mechi hizo, hakufanikiwa kucheza kwa dakika zote na kuishia dakika 847, kama angecheza zote, zingekuwa 1170.

Kisinda mwenye umri wa miaka 20, katika michezo ya ligi ya mabingwa pekee amecheza michezo 11 kwa dakika 749, huku katika Kombe la Shirikisho akicheza michezo miwili kwa dakika 98 ambazo jumla ni 847

Jina la Kisinda limeibukia kwenye usajili wa Yanga hivi karibuni baada ya kuelezwa nyota huyo ni miongoni mwa mapendekezo yaliyoachwa na kocha Luc Eymael

Wadhamini wa Yanga kampuni ya GSM inaelezwa tayari wametuma mwakilishi wake DR Congo kuangalia uwezekano wa kumnasa kinda huyo huku pia ikielezwa bosi huyo amekwenda kumalizana na mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo Heritier Makambo ambaye upo mchakato wa kumrejesha Yanga kutoka klabu ya Horoya AC

Hata hivyo ili kumnasa Makambo, Yanga inapaswa kwenda kumalizana na Horoya kwanza kwani nyota huyo bado ana mkataba wa miaka miwili na miamba hao wa Guinea

Taarifa za ndani zinadai kuwa GSM wamedhamiria kumrejesha nyota huyo wakiwa tayari kuvunja mkataba wake na Horoya

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’