Tutaunda timu ya ubingwa - Eymael

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Apr 2020
Tutaunda timu ya ubingwa - Eymael

Mkufunzi wa Yanga Luc Eymael amependekeza usajili wa wachezaji wanne wa kigeni kuboresha kikosi chake kwa ajili ya kuwania ubingwa wa ligi kuu msimu ujao

Mbelgiji huyo amepania kuipa Yanga ubingwa msimu ujao, amesisitiza kuwa ili kufanikisha hilo wanahitaji kufanya usajili wa wachezaji wenye uwezo wa kufanikisha hilo

Eymael amedokeza kuwa nyota aliopendekeza wasajiliwe wanatoka Mataifa ya Afrika Kusini, Ghana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

"Nipo Ubeligiji lakini kila kitu niliacha kwa viongozi. Kwenye ripoti yangu nimetoa mapendekezo ya wachezaji wanne wa kigeni kutoka kwenye mataifa ya Ghana, Afrika Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo," alisema Eymael

"Kwa msimu ujao kama kocha na benchi la ufundi tumeweka malengo ya kuhakikisha tunachukua ubingwa, hivyo ni lazima usajili wetu uendane na mahitaji ya kuwa na timu imara zaidi ya hii tuliyonayo sasa"

"Nimefanya kazi kwenye Mataifa hayo, nawafahamu wachezaji wa nchi hizo, wanatumia akili na wana kasi na uzoefu. Nadhani tukiwapata wataleta changamoto na ushindani kwenye kikosi chetu"

"Tangu nimefika Tanzania nimeiongoza Yanga kwenye michezo kadhaa licha ya baadhi ya viwanja kuwa katika mazingira magumu kwa wachezaji lakini lazima niwe na kikosi kinachoundwa na nyota wenye uwezo binafsi kama Bernard Morisson kwa ajili ya kusaidia kupata matokeo mazuri katika michezo inayoonekana migumu"

Eymael ameshindwa kurejea nchini kutokana na zuio la kusafiri lililowekwa huko Ubelgiji kutokana na changamoto ya ugonjwa wa Corona

Aidha atakaporejea nchini, napo atakutana na amri ya kukaa karantini kwa siku 14 likiwa ni agizo lililotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli katika jitihada za kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
3h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’