Je Yanga inamuhitaji Mwamnyeto?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Apr 2020
Je Yanga inamuhitaji Mwamnyeto?

Zipo tetesi zinazoihusisha klabu ya Yanga kumuwania beki, nahodha wa Coastal Union Bakari Nondo Mwamnyeto ambaye amekuwa na kiwango bora msimu huu

Inafahamika, kwenye usajili wa dirisha dogo Yanga ilijaribu kumsajili Mwamnyeto lakini wakaachana nae baada ya Coastal Union kutaka dau kubwa

Wapo wanaodhani Yanga itafanya uamuzi sahihi kama itaweza kumsajili beki huyo wa timu ya Taifa kuchukua nafasi ya mkongwe Kelvin Yondani ambaye muda wake wa kuendelea kusakata kabumbu unaelekea ukingoni

Hata hivyo ukiiangalia safu ya ulinzi ya Yanga, ina walinzi wa kati wenye uwezo wa kuziba vyema nafasi ya Yondani

Hakuna aliyedhani kiraka Said Juma Makapu angefikia mafanikio aliyoyapata na kuwa mlinzi wa kutegemewa kwenye kikosi cha Yanga

Makapu alibadilishiwa majukumu kutoka nafasi ya kiungo mkabaji na kocha Luc Eymael baada ya kuvutiwa na aina ya uchezaji pamoja na umbo lake (urefu)

Ukimuondoa Lamine Moro, Yanga pia inao Andrew Vicent, Ally Mtoni na Ally Ally ambaye aligomea kutolewa kwa mkopo mwezi Januari

Walinzi wote wana umri chini ya miaka 27 hivyo Yanga inaweza ikawatumia kwa muda mrefu wakiwa na viwango bora

Hata hivyo Mwamnyeto ni mmoja wa walinzi bora Tanzania kwa sasa, akiwa na umri mdogo, tayari ameshapata uzoefu wa mikiki mikiki ya soka la Kimataifa

Inaeleza Yondani mwenyewe ndiye aliyependekeza Yanga imsajili kinda huyo mwenye umri wa miaka 22 akiamini anaweza kutumika kwa muda mrefu kama ilivyokuwa kwake

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12m ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
30m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
35m ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
10h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
18h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’