Mashabiki Yanga wanamtuza Makambo heshima ya kazi yake

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Apr 2020
Mashabiki Yanga wanamtuza Makambo heshima ya kazi yake

Mashabiki wa Yanga kwa sasa wamekuwa na furaha baada ya kusikia uongozi wa timu hiyo unatarajia kumrejesha mchezaji wao wa zamani, Heritier Makambo katika kipindi cha dirisha kubwa la usajili.

Makambo alijiunga na Horoya FC msimu uliopita kwa mkataba wa miaka mitatu hivyo Yanga kupitia mdhamini wao GSM, yupo tayari kwenda kuvunja mkataba huo na kumrejesha tena kuendelea kuitumikia Yanga ili kuendelea kuwafurahisha mashabiki.

Makambo ambaye awali alijijengea umaarufu mkubwa ndani ya timu hiyo baada ya kufanya vizuri kwa uhodari wake wa kupachika mabao, ambapo alifunga mabao 18 kwenye ligi ndani ya msimu wake wa kwanza na baadae aliachana na mabingwa hao wa kihistoria na kujiunga na Klabu ya Horoya FC ya Guinea.

Ni wazi Makambo hawezi kusahaulika ndani ya Yanga kutokana na kuonesha thamani aliyoitendea timu hiyo kwa msimu uliopita, kiasi cha kuwapa matumanini mashabiki ambao wanaamini kwamba ujio wake utarejesha makali ya Yanga katika kuzifumania nyavu

Msimu huu Yanga pengine ndio imefunga mabao machache zaidi katika kipindi cha miaka 10 iliyopita

Yanga imefunga mabao 31 tu ikizidiwa na idadi ya mabao na timu kama Namungo Fc iliyopanda daraja msimu uliopita

Ni wazi pengo la Makambo linaonekana wazi, kwani safu ya ushambuliaji imekuwa tatizo kubwa kutokana na ubutu wa nyota waliopo kushindwa kufanya kweli

Kama Makambo atarejea na kiwango alichoondoka nacho,bila shaka atawarejeshea mashabiki heshima wanayompa sasa

Kwani kama usajili wake utafanikiwa, atapaswa kuwashukuru mashabiki wa Yanga kwani ndio watakaokuwa wamemrejesha

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’