Moja ya mbinu ambayo mabosi wa Yanga watatumia kuwabaini wachezaji ambao hawafanyi mazoezi kipindi hiki cha mapumziko ya Corona ni kuwapima uzito
Kocha Msaidizi wa Yanga Charles Mkwasa amesema wachezaji wote wa timu hiyo walipewa program za mazoezi ambayo wanapaswa kuyafanya
Amesema ni muhimu kwa nyota hao kutekeleza program hizo kwani wale ambao watapuuzia watakutana na adhabu ikiwemo kukatwa mishahara
"Tumewasisitiza wachezaji wetu wafanye mazoezi huko makwao, tunawafuatilia kwa kuwapigia simu mara kwa mara lakini pia wakirejea tutawafanyia tathmini kila mmoja," amesema Mkwasa
"Mfano ikitokea mchezaji ameongezeka uzito zaidi ya alivyoondoka, tutafahamu hakuwa akifanya mazoezi ipasavyo, hawa tunaweza kuwakata hata mishahara"
Wakati baadhi ya timu zilikuwa zimeanza mpango wa kuvirejesha vikosi vyao kuanza mazoezi, jana TFF ilisisitiza kuwa hakuna timu inaruhusiwa kuandaa mikuanyiko hadi pale Serikali itakapotangaza vinginevyo
Hii ina maana wachezaji wataruhusiwa kurejea kwenye timu zao baada ya Serikali kuondoa katazo la mikusanyiko lililowekwa kuanzia March 17