Nahodha Msaidizi wa Yanga Juma Abdul amewataka mashabiki wa Yanga, wadau wa soka na Watanzania wote kuendelea kuchukua tahadhari wa ugonjwa wa Corona
Kinara huyo wa pasi za mabao kwenye kikosi cha Yanga amesema ni muhimu kwa kila mmoja kuchukua tahadhari kujikinga na ugonjwa huu
"Binafsi naendelea na mazoezi kama alivyoagiza kocha. Katika kipindi hiki kigumu cha ugonjwa wa Corona, nawasihi wanachama na mashabiki wa Yanga kuendelea kuchukua tahadhari kujikinga na ugonjwa huu," amesema Abdul
Serikali ilisitisha shughuli zote za michezo, kufunga shule na vyuo vyote pia kuzuia mikusanyiko kwa muda wa siku 30 ili kudhibiti maambukizi ya ugonjwa huo
Idadi ya waliombukizwa Tanzania imefikia 20, watatu wamepona wakati mtu aliyefariki ni mmoja
ADVERTISE HERE