Jitihada na uvumilivu umeirejesha heshima ya Juma Abdul Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Apr 2020
Jitihada na uvumilivu umeirejesha heshima ya Juma Abdul Yanga

Kama angekuwa ni mchezaji wa kukata tamaa pengine nahodha msadizi wa Yanga Juma Abdul asingeendelea kuonekana ndani ya uzi wa kikosi cha Yanga

Wakati wa kocha Mwinyi Zahera Abdul hakuwa na nafasi kabisa kwenye kikosi cha kwanza

Ukiondoa changamorto ya majeruhi, Mcongomani huyo hakuwa akimuamini kabisa Abdul

Mara kwa mara Zahera alitaja sababu ya kutomtumia Abdul kuwa hakuwa 'fit' na uzito ulikuwa umemzidi

Mwanzoni mwa msimu hasa baada Paulo Godfrey 'Boxer' kuumia, Zahera alidirika hata kumtumia Mapinduzi Balama nafasi ya ulinzi wa kulia licha ya kuwa kwenye benchi alikuwa na Juma Abdul

Mcongomani huyo alianza kumtumia Abdul baada ya presha kubwa ya mashabiki na pale alipoondolewa mwezi Novemba 2019, Mkwasa alimhakikishia Abdul nafasi kwenye kikosi cha kwanza

Tangu wakati huo, Abdul amekuwa nguzo muhimu ya Yanga akiwa kinara wa kutoa pasi za mabao (pasi 5)

Lakini pia takwimu zinaonyesha ndiye mchezaji aliyecheza dakika nyingi zaidi kwenye kikosi cha Yanga msimu huu akifuatiwa na Mghana Lamine Moro

Kama leo mashabiki wa Yanga watapiga kura ya kuchagua mchezaji bora wa msimu wa mabingwa hao wa kihistoria kwa kuangalia mchango wa kila mchezaji, Abdul au Lamine mmoja angestahili kushinda tuzo hiyo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
5h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
9h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
14h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
14h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’