Yanga kukamilisha uwanja wa mazoezi Kigamboni

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Apr 2020
Yanga kukamilisha uwanja wa mazoezi Kigamboni

Wakati mchakato wa ujenzi wa Complex ya Yanga huko Kigamboni ukiendelea,uongozi wa timu hiyo utaanza na kukamilisha uwanja wa mazoezi ili kupunguza gharama za kukodi viwanja, imefahamika

Imeelezwa kampuni ya GSM ambayo ndiyo inayogharamia viwanja na Hostel, itasimamia kukamilishwa kwa uwanja huo ili kuanzia msimu ujao utumike

Kampuni hiyo inatumia hadi Tsh laki tano kwa siku kulipia gharama za viwanja ambavyo Yanga huvitumia

Awali Yanga ilipanga kukamilisha uwanja wake pale Jangwani ambapo zoezi la kumwaga kifusi lilikuwa liko hatua za mwisho

Hata hivyo Serikali iliutaka uongozi wa Yanga usitishe mradi huo kwa kuwa Serikali imeweka mkakati wa kudhibiti mafuriko eneo la Jangwani

Mradi huo utaendelea baada ya Serikali kudhibiti changamoto ya mafuriko Jangwani

"Ni kweli upo mpango wa kutengeneza uwanja wa mazoezi kule Kigamboni. Tulikuwa na zoezi hilo hapa Jangwani lakini Serikali ilituagiza tusitishe kwa kuwa kuna mradi mkubwa wa kudhibiti mafuriko," alisema Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela

"Uzuri kule Kigamboni tunalo eneo zuri ambalo halitachukua gharama kubwa kulikarabati. Tutatengeneza uwanja wa mazoezi wakati mchakato wa mradi mkubwa ukiendelea"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’