Nafanya mazoezi asubuhi jioni napumzika - Kaseke

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Apr 2020
Nafanya mazoezi asubuhi jioni napumzika - Kaseke

Bado haijafahamika ni lini Ligi itaweza kurejea kutokana na janga la virusi vya Corona kuendelea kuitesa dunia

Jana TFF ilitangaza kusogeza mbele muda wa kumalizika ligi kuu ya Vodacom kutoka May 30 hadi Juni 30

Wachezaji wa timu zote wako majumbani wakiendelea na mazoezi binafsi ili kujiweka fiti na tayari kurejea dimbani ligi itakapoanza

Kiungo mshambuliaji wa Yanga Deus Kaseke amesema yeye anatekeleza program aliyoachiwa na kocha Luc Eymael

Kaseka ambaye yuko mkoani Mbeya, amesema ratiba yake ya mazoezi huifanya asubuhi na jioni hupata muda wa kupumzika

"Kwa wachezaji wa Yanga kuna program ambayo kila mchezaji alipewa na kocha, kwa hiyo mimi ndio ninayoifata. Asubuhi nafanya mazoezi ya gym halafu napumzika vizuri kwa kulala, jioni napumzika"

"Kila mchezaji anajua wajibu wake kwa sababu kazi ya mpira ndio inampa kipato cha kuendesha maisha ya familia kwa hiyo naamini kila mchezaji anajitambua na ligi ikirudi kila mtu atakuwa kwenye hali nzuri," aliongeza Kaseke

Kuna wasiwasi kuwa mapumziko haya ya muda mrefu huenda yakaathiri mwenendo wa wachezaji ambapo kwa wale ambao hawatafanya mazoezi ipasavyo wanaweza kuongezeka uzito

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’