Kiungo fundi wa Yanga mwenye udambwi-dambwi wake, Feisal Salum, 'Fei Toto' amesema kuwa kwa sasa anaendelea kufanya mazoezi ili kuwa bora na anachukua tahadhari ya kujilinda na Virusi vya Corona
Fei Toto amesema pamoja na kuwa 'amemis' soka na kuwapa furaha mashabiki wake, lakini ni vyema sasa wakachukua tahadhari kulinda maisha yao kwanza
"Kuna vingi tunavikosa lakini ni muhimu kujali na kulinda afya zetu kwani ni muhimu kuliko kitu kingine chochote"
"Nafanya mazoezi binafsi kulingana na program niliyoachiwa na Mwalimu..Naamini nitakaporejea nitakuwa bora zaidi.." amesema
Baada ya kuanza maisha yake vibaya ndani ya Yanga msimu huu hasa baada ya kocha Luc Eymael kukabidhiwa mikoba, Fei Toto amerejea kibabe kwenye kikosi cha kwanza akimpagawisha Eymael ambaye amempa nafasi katika mechi nne mfululizo
Moja ya mechi alizong'ara zaidi ni ule mchezo dhidi ya Simba ambayo alikuwa bora zaidi kwenye nafasi ya kiungo akimfunika kiungo wa Simba Clatous Chama
