Katika ripoti aliyowaachia mabosi wake Yanga, kocha mkuu wa mabingwa hao wa kihistoria Luc Eymael, amebainisha kuwa anahitaji kikosi cha wachezaji 27 tu
Wachezaji wa ndani ni 24 na magolikipa watatu
Tayari uongozi wa Yanga umeeleza kuanza kufanyia kazi mapendekezo yake ili kuhakikisha msimu ujao Yanga inakuwa na kikosi cha kutwaa ubingwa
Jana Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli alifichua kuwa wanatarajiwa kusajili nyota nne wa kigeni na wakati huohuo wanaendelea na mazungumzo na wachezaji ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu lakini Eymael amependekeza waendelee kubaki
Eymael anatarajiwa kuwasili mwishoni mwa wiki akitokea Ubelgiji ambapo wiki iliyopita alifunga ndoa
ADVERTISE HERE