Mwaka 2011, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ulipokea mgeni, mgeni alipokelewa na mwenyeji wengi kama mafuriko
Alikuwa ni Mnyarwanda, fundi wa mpira, mpira anautuma unaenda, anauita tena unarudi, anaangalia kushoto anapasia kulia
Sio mwingine, ni Haruna Niyonzima aliyetua Yanga akiwa kinda kabisa akitokea klabu ya APR ya Rwanda
Niyonzima alizaliwa huko Gisenyi Februri 5 1990, mwamba huyo alipata mapokezi ya hisia kubwa mno, mashabiki kibao uwanja wa ndege
Katika mahojiano na EFM Radio mapema leo, Niyonzima amesema hadhani kama kuna mchezaji atakuja kupata mapokezi kama yale aliyopata yeye mwaka 2011
"Ilikuwa kitu cha tofauti sana, sijawahi kukiona kwenye mpira. Niliinamisha kichwa nilitokwa na machozi
"Haitatokea tena kama ile, kwangu na kwa mchezaji mwingine yeyote (hapa Tanzania)," alifunguka Niyonzima.
Tangu wakati ule Haruna alijenga uhusiano mzuri sana na Yanga
Mwenyewe amekiri kuwa alipata wakati mgumu sana kuhamia Simba mwaka 2017.
Lakini leo yuko tena Yanga, ameeleza anajisikia faraja sana