Mwaka jana Yanga ilianzisha utaratibu wa kuukaribisha msimu mpya kipekee kwa kuandaa matukio mbalimbali ya kijamii katika wiki iliyopewa jina la Wiki ya Mwananchi
Mwaka huu Yanga itaendelea na utaratibu huo lakini safari hii shughuli hizo zitaanza mapema mwezi wa saba na zitafanyika kwa mwezi mzima
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema mwaka huu wamejipanga kufanya maadhimisho hayo kuwa bora zaidi ya mwaka jana
Siku ya kilele cha maadhimisho hayo, Yanga itacheza mchezo wa kirafiki na moja ya vilabu vikubwa barani Afrika
Mwaka jana ilikuwa icheze na AS Vita ya DR Congo hata hivyo kutokana na mabadiliko ya ratiba ya michuano ya ligi ya mabingwa, wakalazimika kuwaleta Kariobang Sharks, mabingwa wa michuano ya SportPesa
ADVERTISE HERE