Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa 'legendary' Mrisho Khalfan Ngasa maarufu kama 'Uncle'
Ni bahati mbaya sana jina la Ngasa halizungumzwi sana na mashabiki ukilinganisha na mambo makubwa alilolifanyia Taifa la Tanzania
Inaelezwa Ngasa ndiye mfungaji bora wa muda wote timu ya Taifa akiwa ametupia kambani mabao 25
Lakini pia mwaka 2014 akiwa klabu ya Yanga, Ngasa alikuwa mmoja wa wafungaji bora Ligi ya mabingwa barani Afrika akipachika mabao sita
Aliwahi kwenda kufanya majaribio klabu ya West Ham inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza lakini pia huko Marekani klabu ya Seattle Sounders ambapo alipata nafasi ya kucheza mechi dhidi ya Manchester United
Pia mwaka 2015 baada ya kutoka Yanga alisajiliwa na klabu ya Free State Stars ya Afrika Kusini aliyoitumikia kwa misimu miwili kabla ya kupata majeraha yaliyomuweka nje kwa muda mrefu
Ni majeraha hayo ambayo yalisababisha mkataba wake uvunjwe, akaelekea Oman kuitumikia klabu ya Fanja kwa muda mfupi kabla ya kurejea nchini kujiunga na Mbeya City
Yanga ni klabu ya ndoto zake, wakati wote Ngasa amesema huwa anajisikia amani anapocheza klabu ya Yanga
Kwa misimu miwili sasa Ngasa yuko ndani ya kikosi cha Yanga na bado anaonyesha uwezo kuwa na muda mrefu wa kusakata kabumbu
HAPPY BIRTHDAY UNCLE..