Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael atalazimikakurejea mapema ili kuwahi mikiki mikiki ya ligi kuu inayotarajiwa kuendelea baada ya April 17
Eymael aliruhusiwa kwenda kwao ambako wiki iliyopita alifunga ndoa nchini Afrika Kusini kisha kurejea Ubelgji
Atakaporejea Eymael atakaa karantini kwa muda wa siku 14 kulingana na agizo la Serikali kwa wageni wote wanaoingia nchini
Mbelgiji huyo akirejea atakuwa na kazi moja tu, kukiandaa kikosi chake kwa ajili ya kumalizia mechi za ligi zilizobaki lakini kubwa zaidi ni michuano ya kombe la FA
Hivi karibuni Eymael alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kwa sasa hafikirii ubingwa wa ligi kuu kwani tayari wamepoteza nafasi ya kushinda kombe hilo
Hivyo wataweka kipaumbele kwenye michuano ya kombe la FA, wanahitaji kuibuka mabingwa ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao