Ni suala la muda mimi kutua Yanga - Mexime

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Mar 2020
Ni suala la muda mimi kutua Yanga - Mexime

Inaelezwa ile ishu ya kocha wa Kagera Sugar Meckie Mexime kujiunga na Yanga kila kitu kimekamilika na nahodha huyo wa zamani wa timu ya Taifa atajiunga na mabingwa hao wa kihistoria baada ya msimu huu kumalizika

Hivi karibuni Mexime alifichua kuwa alikabidhiwa mkataba wa Yanga tangu mwezi Disemba 2019 lakini alikuwa akisubiri kukamilishwa kwa mambo kadhaa kabla ya kuusaini

Aidha, Mexime amebainisha kuwa Kagera Sugar walimuomba pamoja na uongozi wa Yanga aendelee kubaki na timu hiyo mpaka mwishoni mwa msimu

"Kagera Sugar walikuwa na wasiwasi kama ningeondoka sasa timu ingeweza kuvurugika. Lakini ukweli ni kwamba kila kitu kilikamilika muda mrefu, ni heshima tu mimi kuendelea kuinoa Kagera Sugar," amefunguka Mexime

Kwa sasa Yanga inanolewa na Luc Eymael akiwa kocha mkuu na Charles Mkwasa 'Master' akiwa kocha msaidizi

Kama Mexime atatua Yanga, Mkwasa atampisha kwenye nafasi ya kocha msaidizi na yeye kuwa Mkurugenzi wa ufundi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
3h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’