Bui hajakata tamaa ya kupata nafasi Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Mar 2020
Bui hajakata tamaa ya kupata nafasi Yanga

Kiungo Abdulaziz Makame 'Bui' alianza vyema maisha yake kunako klabu ya Yanga wakati wa kocha Mwinyi Zahera

Alikuwa mmoja wa wachezaji wa kutegemewa kwenye kikosi cha Yanga kilichoshiriki michuano ya ligi ya mabingwa na baadae kombe la Shirikisho

Hata hivyo baada ya kuingia kocha Charles Mkwasa na baadae Luc Eymael, Makame ameshindwa kupenya kwenye kikosi cha kwanza

Pengine ni kutokana na mabadiliko ya mfumo wa uchezaji ambapo makocha hao wamemrejesha nahodha Papy Tshishimbi nafasi ya kiungo mkabaji na hivyo kumfanya Makame akose hata nafasi ya kukalia benchi

Makame amesema pamoja na kuwa jambo hilo linamumiza, lakini amechukua kama changamoto ya kumfanya ajiimarishe zaidi

"Ni changamoto, lakini naamini kila jambo lina wakati wake, mdogo mdogo nitatimiza malengo yangu kwani sijioni kama nimefika na siku zote mwenye njaa ndiye anayetafuta sana," amesema

Hivi karibuni Makame aliingia matatani baada ya inayodaiwa kuwa ni sauti yake kusambaa kwenye mitandao ya kijamii akilalamika kuwa hakupewa mgao baada ya ushindi dhidi ya Simba

Makame hakuwa kwenye kikosi cha wachezaji 18 waliopata nafasi kwa ajili ya mchezo huo

Uongozi wa Yanga umesisitiza kuwa kila mchezaji aliyesajiliwa amepata mgao wake ingawa kiasi walichopata kinatofautiana kulingana na ushiriki wa mchezaji

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
7h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
15h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
22h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’