Yondani ataja siri ya kucheza soka la ushindani kwa muda mrefu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Mar 2020
Yondani ataja siri ya kucheza soka la ushindani kwa muda mrefu

Beki kisiki wa Yanga mkongwe Kelvin Yondani ni mmoja wa wachezaji ambao hata pale atakapostaafu ataacha alama kwa soka la Tanzania

Yondani alisajiliwa na Simba mwaka 2006 akitoka klabu ya Mwanza United ya jijini Mwanza

Mwaka 2012 aliikacha Simba na kujiunga na Yanga, klabu anayoitumikia mpaka sasa

Ana takribani miaka 14 au zaidi anacheza soka la ushindani lakini bado yuko imara kuliko walinzi wengi wadogo

Yondani amesema siri ya kudumu kwa muda mrefu ni pamoja na kufanya mazoezi, kula chakula kizuri na kujipa muda mrefu wa kupumzika

Mkongwe huyo amefunguka kuwa wachezaji wengi wa sasa wanaendekeza sana starehe na ndio maana ni nadra kuwaona wakin'gara kwa muda mrefu

"Mimi nafanya sana mazoezi, lakini pia nakula vizuri. Usiku napata muda mrefu wa kupumzika..hayo mambo ya kujirusha hasa usiku huwa siyapi nafasi," amesema Yondani

"Nawashauri vijana wazingatie hayo, waache kupoteza muda mwingi kwenye kuchat na kujirusha usiku, wazingatie misingi sahihi ili walinde viwango vyao"

Yondani yuko ukingoni kwenye mkataba wake na klabu ya Yanga lakini huenda akaongezwa mwaka zaidi ili aendelee kubaki Jangwani

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
2h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
11h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’