Mashindano ya Challenge kupangua ratiba ya VPL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Nov 2017
Mashindano ya Challenge kupangua ratiba ya VPL
Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wilfred Kidau amesema tayari Tanzania imethibitisha kushiriki mashindano ya Challenge yatakayoanza Novemba 25 hadi Desemba 9 nchini Kenya, huku yakipangua ratiba ya Ligi Kuu Bara.

Kidau amesema awali hawakuyaweka kwenye ratiba mashindano hayo kwa sabababu hawakuwa na uhakika kama yatafanyanyika.

"Tulitengeneza ratiba ya ligi ambayo tuliweka mashindano yote ya kimataifa ili kuepusha ratiba kubadilika.

"Lakini sasa hatuna jinsi kwani tumetaarifiwa ghafla kuwa kutakuwa na mashindano ya Chalenji na kama unavyojua timu yetu ya Taifa inachukua wachezaji wengi wanaoshiriki ligi hivyo lazima ratiba ya ligi ibadilike," alisema Kidau.

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura alisema timu za Taifa zinapokuwa kwenye mashindano lazima ratiba ibadilike hivyo watafanya mabadiliko ya ratiba ya ligi lakini watahakikisha haiathiri fainali ya Kombe la Shirikisho (FA).

"Ratiba ya ligi ya safari hii ni ngumu kwa sababu inatutaka kumaliza ligi Mei 26 mwakani hivyo kwa sababu mashindano ya Chalenji yameibuka tutaangalia jinsi ya kufanya ikiwemo timu kucheza katikati ya wiki tofauti na mwanzo ambapo zilikuwa zikicheza mwishoni mwa wiki pekee," alisema Wambura.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
1h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
5h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
9h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
10h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
13h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’