Tshishimbi akizingua tu, haya majembe yanachukua nafasi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Mar 2020
Tshishimbi akizingua tu, haya majembe yanachukua nafasi

Inaelezwa uongozi wa Yanga tayari umemalizana na nahodha wake Papy Tshishimbi ambaye jana alifika Makao Makuu ya klabu hiyo Jangwani jijini Dar es salaam na kuonana na Katibu MkuuΒ  Dk David Luhago

Taarifa zilizopatikana baada ya kikao hicho zilibainisha kuwa Tshishimbi alikubali kusaini mkataba mpya lakini zoezi hilo atalifanya wiki ijayo

Kulikuwa na kila dalili dalili kuwa Mcongomani huyo alikuwa akijiandaa kuondoka na hivyo uongozi wa Yanga ulikuwa tayari umejipanga ikitokea 'amesepa'

Kuna wachezaji ambao kocha Luc Eymaelalipendekeza wafuatiliwe kwani ni aina ya wachezaji ambao anawahitaji kwenye kikosi chake

Kiungo mkabaji wa Mtibwa Sugar Abdulkarim Humud ni miongoni mwa wachezaji hao

Humid amefichua kuwa alipigiwa simu na viongozi wa Yanga wakiulizia kuhusu Mkataba wake na Mtibwa Sugar ambapo amebainisha kuwa unamalizika mwishoni mwa msimu huu

Nyota huyo aliyeng'ara kwenye kikosi cha Mtibwa amesema hana tatizo kutua Yanga kama atapewa ofa nono

Lakini pia lipo jina la kiungo mkabaji Justice Blay raia wa Ghana, ambaye anachezea Asante Kotoko na timu ya taifa hilo

Inaelezwa Eymael amependekeza nyota huyo asajiliwe, anamfahamu na ana imani kuwa ataongeza nguvu kwenye kikosi chake

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’