Wanayanga wanampenda nahodha Papy Tshishimbi kwa sababu kazi yake inaonekana
Ni mmoja wa wachezaji wanaofahamu thamani ya kucheza klabu ya Yanga
Haishangazi kuona kila mmoja anataka aongezwe mkataba ikielezwa tayari alishazungumza na GSM lakini ameweka masharti kabla ya kusaini
Inaelezwa Tshishimbi ametaka mkataba wa miaka miwili huku akiomba mshahara wa Tsh Milioni 18 na dau la usajili linalofikia Tsh Milioni 150!
Pamoja na kutambua ni mchezaji muhimu lakini nadhani dau hili analotaka ni kubwa sana
Yanga inahitaji huduma yake lakini sidhani kama itakuwa kwa gharama hiyo
Lakini pia, kwa ziara anazofanya kwenye vyombo mbalimbali vya habari, kauli zake hazionyeshi dalili nzuri kama ni mchezaji anayetaka kuendelea kubaki Yanga
Mwisho wa siku lolote linaweza kutokea, lakini Yanga haiwezi kutetereka ikitokea ameamua kuondoka kwani nyota wengi wazuri kama yeye au zaidi yake walicheza na kuondoka Yanga na timu imebaki palepale