Wanayanga wasubiri kauli ya Dk Msolla

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
25 Mar 2020
Wanayanga wasubiri kauli ya Dk Msolla

Wanayanga wanasubiri kusikia kauli ya Mwenyekiti wao Dk Mshindo Msolla baada ya GSM kutangaza kusitisha huduma walizokuwa wakizitoa kwa klabu ya Yanga na wakati huohuo wakibainisha kubaki na jukumu la kutengeneza na kusambaza jezi tu

Jana Yanga ilikanusha tuhuma zilizotolewa na Mwanachama Juma Magoma kuwa kuna masuala mengi ndani ya uongozi wa Dk Msolla hayaendi sawa lakini pia akatahadharisha kuwa GSM walikuwa mbioni kujiondoa kutokana na mgongano uliopo

Hili limetimia, ni wazi Wanayanga wataamini yale yaliyosemwa na Magoma kuwa yote yana ukweli kama Mwenyekiti hatajitokeza kuzungumza na kuweka mambo sawa

Lakini pia Wanayanga wanataka kusikia uongozi wake umejipangaje kuhakikisha hakuna changamoto zinajitokeza baada ya GSM kujiondoa

Inafahamika, GSM ndio waliokuwa wakilipa mishahara ya makocha wote, wachezaji lakini pia waligharamia kambi, vifaa na viwanja vya kufanyia mazoezi tangu mwezi wa kwanza

Kwa ufupi, GSM walihusika kwenye kila hatua kurejesha amani ya klabu ya Yanga tangu kuibuka lile sakata la wachezaji kuvunja mikataba kutokana na madai ya mishahara

Β 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
26m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’