Nahodha wa Yanga Papy Tshishimbi amefichua kuwa kama Tanzania itahitaji huduma yake kwenye timu ya Taifa yuko tayari kufanya hivyo
Tshishimbi ambaye alijiunga na Yanga mwaka 2017 akitokea Mbabane Swallows ya eSwatini, amesema hajawahi kucheza timu ya Taifa ya DR Congo hivyo hataona shida kama atapewa nafasi kuichezea timu ya Taifa ya Tanzania
"Mimi sijawahi kupata nafasi kuichezea timu ya Taifa langu DRC, hivyo ikitokea nimepewa nafasi ya kuchezea timu ya Taifa ya Tanzania, niko tayari," amesema Tshishimbi
Tshishimbi amekuwa mmoja wa wachezaji muhimu wa kikosi cha Yanga tangu alipojiunga na timu hiyo
Pengine anaweza kuwa msaada kwa timu ya Taifa kama Tanzania itaamua kumpa uraia ili achezee timu ya Taifa
ADVERTISE HERE