Usajili wote atafanya Eymael - Mwakalebela

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Mar 2020
Usajili wote atafanya Eymael - Mwakalebela

Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kuwa hawatamuingilia kocha Luc Eymael katika usajili wa kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao

Akizungumza juzi baada ya kikao cha kwanza cha Kamati ya Utendaji mwaka huu, makamu Mwwnyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela alisema wamemwachia Eymael jukumu la kutafuta wachezaji wao kazi yao itakuwa moja tu, kuhakikisha wachezaji hao wanasajiliwa

"Jukumu la usajili tumemuachia kocha. Yeye ndio anafahamu wachezaji wazuri ambao wanaweza kuisaidia timu. Sisi kazi yetu itakuwa moja tu, tunawaleta," alisema

Hata hivyo Mwakalebela amesema usajili wa msimu huu wataongeza umakini ili kuhakikisha makosa waliyofanya msimu uliopita hayajitokezi

"Hatuwezi kurudia makosa, Eymael anafanya majukumu yake na anapomuona mchezaji ambaye atakuja kusaidia timu, viongozi wanaenda kumalizana na mchezaji au klabu kama bado ana mkataba nayo"

Msimu uliopita Yanga ilimuachia majukumu yote ya usajili aliyekuwa kocha Mkuu Mwinyi Zahera lakini nyota wengi aliowasajili walikuwa na uwezo wa kawaida

Mwezi Januari Yanga ililazimika kuvunja mikataba ya baadhi ya wachezaji wa kigeni na kufanya usajili mwingine

Wachezaji walioachwa baada ya kuitumikia Yanga kwa miezi sita tu ni Sadney Urikhob, Juma Balinya, Maybin Kalengo, Mustafa Selemani na Issa Bigirimana

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10m ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
3h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
8h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
8h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE β†’