Msimu wa 2017/18 uongozi wa klabu ya Yanga walianzisha mradi wa jarida la klabu hiyo ambalo lilipaswa kutoka kila mwezi mara moja
Mradi huo ulisimamiwa na aliyekuwa Afisa Habari Dismas Ten ambaye sasa ni Afisa Masoko
Hata hivyo baada ya kutoa toleo moja tu, mradi huo haukuendelea huku sababu za mradi huo kufa zikiwa hazikuwekwa wazi
Uongozi wa Yanga umebainisha kuwa wako kwenye mpango wa kuufufua mradi huo ambao utaingizia Yanga mamilioni
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema mchakato wa kulirejesha jarida hilo uko kwenye hatua za mwisho na kuwataka mashabiki wa Yanga wakae mkao wa kula
Jarida hilo litasheheni taarifa za kina kuhusu masuala mbalimbali yanayoihusu klabu ya Yanga
ADVERTISE HERE