Morrison, Tshishimbi kuiponza Simba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Mar 2020
Morrison, Tshishimbi kuiponza Simba

Klabu ya Simba ilikuwa imekomaa kwelikweli kumsajili fundi mtembea juu ya mpira Bernard Morrison ambapo uongozi wa Yanga kupitia wadhamini wao GSM walilazimika kuchukua hatua kumpa mkataba wa miaka miwili

Lakini pia nahodha Papy Tshishimbi alikuwa akiwaniwa na timu hiyo licha ya kuwa mkataba wake ulikuwa bado una mwaka mmoja

Sasa GSM wameandaa 'pigo takatifu' kwa mabingwa hao wa ligi kuu kwa 'kutia maguu' kambini kwao

Achana na kina Yusufu Mlipili na Said Ndemla ambao kila msimu wamekuwa wakitajwa kuwaniwa na Yanga pasipo ukweli wowote

Katika nyota hawa watatu Clatous Chama, Jonas Mkude na Deo Kanda kuna jambo litatokea!

Inaelezwa wote mikataba yao inamalizika mwezi Juni na wote mpaka sasa wamegoma kuongeza mikataba mipya!

Kocha wa zamani wa Yanga Mwinyi Zahera ambaye ameweka makazi yake nchini, inaelezwa ndiye aliyeachiwa jukumu la kumnasa Kanda ambaye pia klabu yake ya TP Mazembe inafanya jitihada za kumpa mkataba mpya

Kanda anaitumikia Simba kwa mkopo, lakini mwezi Juni atakuwa huru kwani mkataba wake utakuwa umemalizika

Msimu uliopita Simba ilisajili wachezaji watatu wa Yanga Beno Kakolanya, Ibrahim Ajib na Gadiel Michael

Ukiondoa Kakolanya ambaye makubaliano ya pande zote yalifikiwa kuvunja mkataba wake, Ajib na Gadiel wao waligoma kusaini mikataba mipya na wakajiunga na Simba

Ingawa ni uamuzi ambao huenda wakawa wanaujutia kwani wamekosa nafasi kwenye timu hiyo huku ukiibuka uvumi kuwa kocha wa Simba amependekeza Ajib apelekwe timu ya vijana ili akajiimarishe

Akiwa Yanga, Ajib alikuwa kinara wa pasi za mabao msimu uliopita..!

Lakini msimu huu wajiandae kisaikolojia kwani GSM wametenga huko Yanga zaidi ya Bilioni moja na nusu kwa ajili ya usajili

Mhandisi Hersi Saidi kinara wa 'kusinya' amesema hakuna mchezaji ambaye watamtaka watashindwa kumsajli

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
5h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’