Kuanzia msimu ujao, Bodi ya Ligi imeandaa utaratibu wa kuzibana timu zenye madeni sugu ya wachezaji kwa kuzizuia kushiriki ligi kabla ya kumaliza madeni hayo
Mtendaji Mkuu wa Bodi ligi kuu Tanzania Bara, Almas Kasongo amebainisha kuwa hakuna timu ya Ligi Kuu itaruhusiwa kushiriki ligi kama itakuwa, inadaiwa na wachezaji wake
Lakini pia ili timu iwe na sifa ya kushiriki ligi kuu ni lazima iwe na Mtendaji Mkuu (CEO), Mwanasheria, Mtaalamu wa Fedha na Afisa Habari Mwenye Sifa
Suala la madeni ya wachezaji limekuwa tatizo kwa timu nyingi zinazoshiriki ligi kuu
Na hili hutokana na kuzidiwa na gharama za uendeshaji kwa kuwa timu nyingi hutegemea zaidi mapato ya milangoni, fedha za wadhamini na wafadhili
ADVERTISE HERE