Uongozi wa klabu ya Yanga jana ulikuwa na kikao cha kujadili masuala mbalimbali yanayoihusu klabu hiyo
Pamoja na mambo mengine, mabosi hao wa Yanga waliandaa mkakati wa kuhakikisha timu inaweza kupata ushiriki wa michuano ya Kimataifa kwa kutwaa taji la FA timu ikiwa imetinga robo fainali
Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema wameweka malengo hayo baada ya kupoteza nafasi ya kutwaa ubingwa msimu huu
Msimu ujao ni timu mbili tu kutoka Tanzania zitashiriki michuano ya CAF baada ya Libya kuiondoa Tanzania nafasi ya 12 kwenye viwango vya CAF
Aidha mabosi hao walijadili mpango mkakati wa usajili pamoja na kuwajadili nyota walioagizwa kuandika barua wakituhuma na makosa ya utovu wa nidhamu hasa baada ya kukosa safari Lindi
Mwakalebela amesema kocha mkuu wa Yanga Luc Eymael ametoa msamaha kwa wachezaji wote