Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo inatupa karata yake ya mwisho kujaribu kusata tiketi ya kutinga robo fainali ya michuano ya Cosafa inayoendelea nchini Afrika Kusini pale itakapoivaa Mauritius.
Stars inaongoza kundi A baada ya kujikusanyia alama nne na mabao mawili ikifuatiwa na Angola yenye alama nne na bao moja.
Ni timu kinara wa kundi tu ndiyo itatinga robo fainali hivyo ni lazima Stars ishinde mchezo wa leo kwa idadi kubwa ya mabao kadiri itakavyowezekana ili kuizidi Angola ambayo nayo itakuwa inasaka ushindi dhidi ya Malawi.
Kinara wa kundi A atatinga robo fainali na huenda akachuana na Afrika Kusini katika hatua hiyo.

ADVERTISE HERE