Uongozi wa klabu ya Yanga umetamba kuweka rekodi ya mauzo ya jezi ya mshambuliaji Bernard Morrison raia wa Ghana
Tangu walipotengeneza jezi maalum za mshambuliaji huyo na kuziuza kwa bei ya Tsh 50,000, nakala zaidi ya 5,000 zimeuzwa
Hii ina maana GSM wameweza kuingiza mapato ambayo sio chini ya Tsh Milioni 250 kwa mauzo ya jezi za Morrison tu
Sasa kama kungekuwa na Ma-Morrison wanne tu, kiasi cha Tsh Bilioni 1 au zaidi kingepatikana
Mkakati sasa ni kuhakikisha nyota wakali wanatua Yanga ili kuendelea kuimarisha biashara ya mauzo ya jezi
Hivi ndivyo timu kubwa zinavyoingiza mkwanja huko Ulaya
Nakumbuka klabu ya Juventus ilipomnunua Cristiano Ronaldo kutoka Real Madrid ilihitaji wiki moja tu kurudisha pauni Milioni 105 walizotumia kumnunua mwamba huyo kwa mauzo ya jezi yake tu
Kutokana na mahitaji kuendelea kuwa juu, jezi maalum ya Morrison sasa inauzwa Tsh 70,000/- lakini pia zipo nakala nyingine ambazo zinapatikana kwa bei elekezi
Β