Wadhamini wa Yanga kampuni ya GSM wamedhamiria kutengeneza kikosi cha mauaji mapema kuondokana na zile adha za wachezaji wasumbufu
Ni hivi, kwa sasa huko jangwani kuna zoezi la kuhuisha mikataba iliyomalizika ya nyota ambao kocha Luc Eymael amependekeza wapatiwe mikataba mipya
Mwezi Juni zile vurugu za wachezaji kuringa kusaini mkataba ili waongezewe dau hazitakuwepo tena kwani wakati huo zoezi litakalokuwa likifanyika ni la kuongeza nyota wapya tu
Yanga imeamua 'kuwapiga pini' nyota wake mapema ili hata ikitokea mchezaji ataringa kusaini mkataba, ataachwa na nafasi yake kutafutwa nyota mwingine
Kwa utaratibu unaotumika sasa hakutarajiwi matukio kama yale yaliyofanywa na kina Gadiel Michael ambaye alipewa mkataba lakini baadae akagoma kusaini siku mbili kabla ya dirisha la usajili kufungwa na kutimkia Simba