Tetesi za klabu ya Simba kumuwania mshambuliaji wa Yanga Bernard Morrison zimeanza tena ikielezwa mabosi wa klabu hiyo wanamshawishi nyota huyo asaini kwao
Awali Morrison alitua Yanga kwa mkataba wa miezi sita lakini taarifa za uhakika ni kuwa mazungumzo ya kumuongeza mkataba yalishafanyika na kilichokuwa kikisubiriwa ni yeye kusaini mkataba mpya wa miaka miwili
Morrison ni mchezaji muhimu wa kikosi cha Yanga, ni wazi Yanga haiwezi kumuachia akaondoka kirahisi
Uongozi wa Yanga unafahamu jitihada zinazofanywa na Simba ambapo wametahadharisha kuwa watapeleka malalamiko TFF kama wataendelea kumsumbua mchezaji huyo
Lakini pia Morrison amekuja Yanga kutokana na ushawishi wa kocha Luc Eymael ambaye ameweka bayana kuwa mchezaji huyo anamuhitaji sana, mwishoni mwa msimu ataongeza nyota wengine ambao pamoja nae wataiongezea makali Yanga
Imekuwa ni kawaida tetesi kama hizi kusikika kuelekea dirisha la usajili, lakini kwa hili la Morrison zitabaki kuwa tetesi tu