Kiungo mshambuliaji Benard Morrison amekuwa mchezaji wa kwanza kuwekwa chini ya uangalizi baada ya kuonyesha dalili ya maambukizi ya virusi vya Corona
Morisson aliondolewa kwenye kambi ya Yanga tangu juzi ingawa jana uongozi wa Yanga ulivunja kambi na kuwaruhusu wachezaji wote kurudi majumbani
Mbali na Morrison, nyota mwingine ambaye inaelezwa amefanyiwa vipimo vya ugonjwa huo ni Ditram Nchimbi
Mpaka sasa Serikali imethibitisha watu watatu wamekutwa na maambukizi ya ugonjwa huo nchini huku wengine 26 wakiwekwa chini ya uangalizi mkoani Arusha
Serikali imesitisha shughuli zote za michezo kwa muda wa mwezi mmoja pamoja na kufunga shule zote na jana tamko jingine likitolewa na Waziri Mkuu kufunga vyuo vya elimu ya juu
ADVERTISE HERE