Eymael apewa rungu la kuisuka upya Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Mar 2020
Eymael apewa rungu la kuisuka upya Yanga

Kabla ya mchezo dhidi ya Namungo Fc, Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael alitoa malalamiko kwa baadhi ya wachezaji wa timu hiyo hawaipi heshima nembo ya Yanga vile inavyopaswa

Alichukizwa na kitendo cha baadhi ya nyota kugoma kusafiri na timu mkoani Lindi akikifananisha kitendo hicho na usaliti kwa klabu

Mbelgiji huyo alibainisha kuwa katika maisha yake ya ukocha hakuwahi kukutana na kitu kama hiki, akieleza kushangazwa na utamaduni huu wa wachezaji kuchagua mechi

Sasa jana uongozi wa Yanga ulitarajia kukutana nae ambapo pamoja na mambo mengine, ni kujadili matukio hayo ya utovu wa nidhamu

Huenda mabadiliko mengine makubwa ya kikosi yakashuhudiwa mwishoni mwa msimu kwani Mbelgiji huyo amepewa rungu kubadili mambo kadhaa pale Jangwani

Wachezaji watovu wa nidhamu hawatakuwa na nafasi kwenye kikosi chake msimu ujao huku ikielezwa pia GSM wamempa ruhusa kusaka wachezaji ambao anadhani wataisaidia Yanga kulingana na mapungufu yaliyopo

Katika moja ya mahojiano yake hivi karibuni, Eymael alieleza kuwa kama angejiunga na Yanga mapema kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa, angesajili wachezaji watatu

Lakini alifanikiwa kumsajili mchezaji mmoja tu Bernard Morrison huku akitamba kuwa msimu ukimalizika atasajili nyota wengine ambao anawafahamu ni hatari zaidi ya Morrison

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
2h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
11h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’