Wachezaji hawakujituma tangu mazoezini - Luc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Mar 2020
Wachezaji hawakujituma tangu mazoezini - Luc

Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema alikuwa na hofu timu yake isingefanya vizuri kwenye mchezo dhidi ya KMC leo baada ya kutoridhishwa na morali ya wachezaji mazoezini

Akizungumza na wanahabari baada ya mchezo huo uliomalizka kwa Yanga kufungwa bao 1-0 na KMC, Eymael amesema wachezaji wake walijisahau baada ya ushindi dhidi ya Simba

"Nilikuwa na wasiwasi kuelekea mchezo huu kwani sikuridhishwa na kile nilichokuwa nikikiona mazoezini," alisema Luc

"Bahati mbaya kwa hapa Tanzania, timu ikishinda dabi wachezaji wanaona kama wametwaa kombe la dunia. Niliwatahadharisha wachezaji wangu kuhusu umuhimu wa kujituma ili kupta ushindi kwani mechi ya Simba haina tofauti na mechi nyingine zote tunasaka alama tatu"

"Ni jambo baya sana kupoteza mchezo leo lakini wakati mwingine mambo haya hutokea, tunajipanga kwa ajili ya mchezo unaofuata"

Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuelekea mkoani Lindi kesho tayari kwa mchezo dhidi ya Namungo Fc ambao utapigwa Jumapili

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
19h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’