Afisa Msemaji na Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi uwanja wa Uhuru kuiunga mkono timu yao kwenye mchezo dhidi ya KMC
Miamba hao wa soka kutoka jiji la Dar es salaam watakuwa na nafasi ya kuendelea kuwapa furaha mashabiki wao ambao bado wanahanikiza ushindi waliopata dhidi ya watani zao Simba Jumapili iliyopita
Yanga inahitaji kushinda mchezo huo ili kuendelea kuwaweka katika presha vinara wa ligi Simba ambao kimahesabu wana nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa
Mchezo utapigwa kuanzia saa kumi kamili jioni
ADVERTISE HERE