Kikosi cha Yanga leo kimekamilisha maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC
Mchezo huo utapigwa kesho Alhamisi kwenye uwanja wa Uhuru
Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema vijana wake wako tayari kuelekea mchezo huo ambao ana matumaini watafanya vizuri
"Wachezaji wapo tayari na kila mmoja anatambua majukumu yake nina imani kila kitu kitakuwa sawa.
"Tumedhamiria kufanya vizuri katika michezo yote iliyobaki pamoja na kuwa tuna nafasi ndogo ya kuwa mabingwa, basi tujihakikishie kumaliza nafasi ya pili" amesema
Baada ya mchezo huo Yanga inakabiliwa na mchezo wa kiporo dhidi ya Namungo Fc ambapo italazimika kusafiri wilayani Ruangwa tayari kwa mchezo huo ambao utapigwa Jumapili March 15
ADVERTISE HERE