Nahodha wa Yanga, Papy Tshishimbi amevutiwa na maisha ya Tanzania na kusema yupo tayari kubadilisha uraia wake ilia pate nafasi ya kuichezea timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'.
Tshishimbi raia wa DR Congo alisema iwapo atapata nafasi ya kuitwaa Taifa Stars yupo tayari kubadilisha uraia wake.
Mcongomani huyo amesema nje na soka anafurahia maisha ya Tanzania namna wanavyopenda soka ikiwa ni sambamba na nchi yenyewe ilivyo na maisha ya kawaida.
"Mbali na soka mimi napenda maisha ya Tanzania pia nafuraishwa na umoja na upendo uliopo kutoka kwa wananchi wa nchi hii hawana ubaguzi wanampenda kila mtu na wanaushirikiano mzuri tofauti na mataifa mengine niliyowahi kucheza," alisema Tshishimbi.
Tshishimbi aliongeza kuwa mbali na kuwa na mpango wa kufanya hivyo kwa upande wake endapo ataweza kufanikisha hilo basi hadi familia yake itatakiwa pia ufuate uraia wake ili waweze kuishi pamoja Tanzania.