Makala hii imeandikwa na Baraka Mbolembole
Kiwango cha juu kutoka kwa kocha Mzambia, George Lwandamina katika machaguo ya wachezaji, mbinu na usomaji wa mchezo kumempa ‘heshima kubwa’ kocha huyo wa zamani wa Zesco United. Licha ya kuendelea kusubiri kupata ushindi wake wa kwanza katika ‘Dar es Salaam-Pacha’, Lwandamina ameonyesha matarajio makubwa zaidi ya klabu katika siku za mbeleni.
Alijiamini wakati akifanya usajili katikati ya mwaka huu na hakuonekana kutetereka licha ya timu yake kupoteza robo tatu ya kikosi cha kwanza.
Kuanza na wachezaji 9 wazawa katika mchezo dhidi ya mahasimu wao Simba siku Jumamosi iliyopita huku kikosi cha Yanga kikicheza bila, Deogratius Munishi (sasa anacheza Afrika Kusini,) Mwinyi Haji (amepoteza namba kwa kijana mpya kikosini Gadiel Michael,) Vicent Bossou (ameondoka baada ya kumalizika kwa mkataba wake,) nahodha, Nadir Haroub (amepoteza namba yake mbele ya Vicent Andrew,) Saimon Msuva (sasa anacheza Morocco,) Haruna Niyonzima (yupo Simba hivi sasa,) Thaban Kamusoko (anasumbuliwa na majeraha,) Amis Tambwe (anasumbuliwa na majeraha,) na Deus Kaseke (sasa anaichezea Singida United) Kwa jicho la kawaida unaweza usione kitu lakini haya ni mapinduzi makubwa yamefanywa Lwandamina na timu yake ya ushindi.
Kiwango cha timu katika michezo mitatu iliyopita kimeondoa ile dhana kuwa mabingwa hao watetezi wataangusha ubingwa huo msimu huu. Inawezekana lakini kwa namna timu mpya ya Lwandamina ilivyocheza vs Simba ni ngumu sana kwa klabu nyingine kuutoa ubingwa huo pale Mitaa ya Twiga na Jangwani.
Na kwa namna mambo yanavyoonekana sitashangaa mabingwa hao mara 27 wa kihistoria wakishinda taji hilo hata kufikia mara tano mfululizo. Kikosi hiki kipya chenye magolikipa, Youthe Rostand, Beno Kakolanya, Ramadhani Kabwili. Walinzinzi, Juma Abdul, Ramadhani Kessy, Gadiel, Mwinyi, Nadir, Vicent, Kelvin Yondan, Pato Ngonyani.
Viungo, Said Juma Makapu, Juma Mahadhi, Papy Tshishimbi, Kamusoko, Pius Buswita, Rafael Daud, Geofrey Mwashuiya, Emmanul Martin, Ibrahim Ajib, na washambuliaji, Matheo Anthony, Ngoma, Tambwe na Obrey Chirwa kinahitaji maingizo machache tu pale kocha atakapotaka ili kiendelee kutawala VPL.
Azam FC wanaweza kuwa kikwazo kikubwa zaidi kwa Yanga. Mabingwa hao mara moja wa kihistoria wameshatambua baadhi ya makosa yaliyowafanya ‘kushindwa kukua’ zaidi mara baada ya kutwaa VPL pasipo kupoteza mchezo msimu wa 2013/14.
Azam FC kama ilivyo Yanga wamefanya usajili wa wachezaji vijana wenye tamaa ya kukua haraka kimpira, wana benchi zuri la ufundi na sasa watendaji wa juu wa klabu wanafanya kazi zao na kutekeleza yanayotakiwa na watu wa ufundi. Simba haiwezi kutwaa ubingwa msimu huu kwa maana walisajiliwa wachezaji na kusahau kusajili benchi zuri la ufundi na kwa vile kila kitu waliamini katika fedha wakajikuua wakishindwa kutengeneza timu na badala yake wamesajili wachezaji wazuri ambao ubora wao uwanjani unatia shaka.
Yanga, Azam FC walisajili timu zao kwa mtazamo wa baadae licha ya kwamba kama klabu, tena klabu kubwa ni lazima washindanie mataji hata katika michuano ya sasa. Kuendelea kusajili wachezaji ghali tena ‘wa msimu mmoja’ kutaendelea kuwapotezea muda Simba na wataendelea kuachwa hatua nyingi na mahasimu wao Yanga ambao sasa sajili zao zinasimamiwa zaidi na makocha si wanachama, viongozi au wajomba wa wachezaji.
Nilikuwa 50/50 kuhusu uwezo wa Lwandamina lakini sasa napandisha alama za ubora wake kufikia 70% na zitakapofikia 90% Yanga watakuwa wanalipa kisasi kikubwa kwa Simba. Kuifunga Singida United ikicheza kwa mara ya kwanza pale Namfua Stadium chini ya Mholland, Hans van der Pluijm upande si sababu, ila Lwandamina amewaonyesha na kuwafundisha Simba namna ya kutengeneza timu bora. Kuna siku atawaadhibu.

ADVERTISE HERE