TFF tendeni haki, lindeni wachezaji wenu wa timu ya Taifa - Ridhiwani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Mar 2020
TFF tendeni haki, lindeni wachezaji wenu wa timu ya Taifa - Ridhiwani

Mbunge wa Chalinze ambaye ni Mwanachama wa klabu ya Yanga Ridhiwani Kikwete amelitaka shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kulinda wachezaji kwa kutenda haki na kuhakikisha sheria 17 za mpira wa miguu zinazingatiwa

Ridhiwani ametoa maoni yake kufuatia tukio la Clatous Chama wa Simba kumkanyaga kwa makusudi kiungo wa Yanga Feisal Salum kwenye mchezo wa watani wa jadi uliopigwa juzi kwenye uwanja wa Taifa ambao ulimalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0

Ameitaka TFF ichukue hatua bila ya kusubiri malalamiko kutoka kwa klabu ya Yanga

Ikumbukwe tukio kama hilo lilifanywa na beki wa Simba Paschal Wawa dhidi ya Ditram Nchimbi kwenye mchezo wa kwanza baina ya timu hizo ambao ulimalizika kwa matokeo ya sare ya mabao 2-2

Hata hivyo TFF haikumchukulia hatua yoyote Wawa licha ya kuonekana dhahiri akimkayaga Nchimbi kwa makusudi

"Na hili nalo ⁦β€ͺTFF mnataka ⁦β€ͺYanga waje kulalamika? Lindeni Wachezaji wa timu ya taifa. Ninyi ndiyo wasimamizi wa mpira Tanzania. Tendeni haki kama kauli mbiu inavyosema ' Our Game Is Fairplay', Be fair," aliandika Ridhiwani kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram

Jana Chama aliomba radhi kwa tukio hilo lisilo la kiungwana alilomfanyia Fei Toto

Wadau wamempongeza Chama kwa kuwa muungwana lakini bado TFF ina nafasi yake ya kuchukua hatua ili kuhakikisha matukio haya hayaendelei kujitokeza

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
3h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’