Baada ya mshikemshike wa mpambano wa watani wa jadi kumalizika, Ligi Kuu ya Vodacom inaendelea leo ambapo inaingia mzunguuku wa 28
Mechi saba zinatarajiwa kupigwa katika viwanja mbalimbali
Yanga iliyoibuka kidedea juzi kwenye mchezo dhidi ya Simba, itashuka dimbani siku ya Alhamisi kuwakabili KMC
Watani zao Simba ambao ndio vinara wa ligi hiyo, wao watashuka dimbani kesho Jumatano kuwakaribisha Singida United katika mchezo ambao utapigwa uwanja wa Uhuru
Mechi zote za leo zitapigwa saa kumi jioni

ADVERTISE HERE