Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amemkabidhi baiskeli mpya Twalib Kimbwembwe kutoka wilayani Kilwa mkoa wa Lindi ambaye amekuwa gumzo baada ya uchambuzi wake wa mchezo dhidi ya Simba kufanikiwa
Yanga iligharamia safari ya Twalib pamoja na mzazi wake kuhakikisha wanaushuhudia mchezo dhidi ya Simba 'mbashara'
Twalib alitabiri kuwa Yanga ingeondoka na ushindi wa mabao 2-0, hata hivyo Yanga ikafanikiwa kushinda bao 1-0
Yanga pia imegharamia safari ya bwa mdogo huyo kurudi Lindi
ADVERTISE HERE